AUNTY: NILIISHI MAISHA MACHAFU NIPATE KIKI

Share this story


Nyota wa filamu nchini Gwantwa Ezekiel (Aunty Ezekiel) amefunguka kuwa kipindi cha nyuma kabla ya kupata watoto alikuwa akijiachia sana kwa lengo la kutafuta kiki na wala hakuwa na woga wa kufa kwani hakuwa anategemewa na watu.

Aunty Ezekiel alisema hayo na kudai kuwa alikuwa akivaa vibaya, kukaa kwenye pozi mbovu mbovu na kuwa na skendo mbalimbali kwa lengo la kutafuta kiki na kufahamika zaidi lakini saizi yeye hafanyi tena mambo hayo kwani amekuwa akiogopa kifo kwa kuwa anatambua nyuma ana watoto ambao wanamtegemea na wanategemea malezi yake, ndiyo maana ameamua kuachana na mambo hayo.

“Kwa sasa nimeacha kiki za ajabu ajabu saizi naangalia maisha ya familia, saizi nimekuwa mama naangalia vitu kwa upande mwingine kesho na kesho kutwa wanangu wamekua, wakute matukio hayo, ohh mama yako alivaa kichupi, mama yako alikuwa hivi alikuwa vile wataiga nini watoto kutoka kwangu..?? Kwa hiyo saizi naangalia mara mbili ya pale nilipokuwa mwanzo.

Hata zamani nilikuwa ni mtu ambaye nasema aah si tunaishi mara moja tu hivyo kesho na kesho kutwa nikifa nasema potelea mbali lakini saizi nakiogopa kifo kutokana na kwamba nina watu nyuma yangu ananitegemea”- alisema @auntyezekiel


Share this story

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Previous post VATICAN : MIPANGO YA MAZISHI YA PAPA FRANCIS YAENDELEA