Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Tundu Lissu ameachiwa kwa dhamana baada ya kukamatwa Jeshi la Polisi mkoani Arusha
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu na wenzake wameachiwa kwa dhamana na Jeshi la Polisi Mkoani Arusha baada ya kukamatwa kwa tuhuma za kufanya mikusanyiko isiyokuwa halali na kuwazuia Askari kufanya kazi yake.
Akiongea na Waandishi wa Habari baada ya kuachiwa Lissu amesema alikamatwa na kupelekwa Kituo cha Polisi Monduli na baadaye Kituo Kikuu cha Polisi Arusha ambapo amesema amegoma kutoa maelezo hadi kesho September 11,2023 atakaporudi Kituo cha Polisi saa tatu asubuhi kama alivyoambiwa.