FIFA ILIKOSEA QATAR KUWA MWENYEJI WA KOMBE LA DUNIA

Share this story

Rais wa zamani wa FIFA, Sepp Blatter, amedai hakutaka shughuli ya kandanda ya 2022 ifanyike Qatar kwa kuwa ni Nchi ndogo kuweza kusimamia Michuano hiyo

Sepp Blatter alikuwa rais wa FIFA mwaka 2010 wakati Kombe la Dunia lilipotolewa kwa Urusi na Qatar; Blatter aliliambia gazeti la Uswizi la Tages-Anzeiger: “Chaguo la Qatar lilikuwa kosa. Kwa hakika tulikubaliana katika kamati kuu kwamba Urusi inapaswa kupata Kombe la Dunia la 2018 na Marekani lile la 2022.”

Uamuzi huo wa Qatar umekumbwa na utata, ikiwemo madai ya ufisadi na ukiukaji wa haki za binadamu, tangu ulipotangazwa kwa mara ya kwanza.

Blatter, ambaye aliongoza FIFA kwa miaka 17, pia amekumbwa na tuhuma za ufisadi wakati wa uongozi wake. Aliondolewa kosa la udanganyifu na mahakama ya Uswizi mwezi Juni. Waendesha mashtaka wamekata rufaa dhidi ya uamuzi huo.

Michuano ya Kombe la Dunia inatarajiwa kuanza Novemba 20 hadi Desemba 18, 2022.

Qatar itakuwa nchi ya kwanza katika Mashariki ya Kati kuandaa michuano hiyo.


Share this story

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Previous post Mahakama yaamuru marubani kurejea kazini Jumatano
Next post Ruto Seal Visa-Free Deal With South Africa’s President Ramaphosa