Mwandishi wa habari wa Urusi anauza Tuzo la Amani la Nobel kwa dola milioni 103.5 kusaidia watoto wa Ukraine

Share this story

Mwandishi wa habari wa Urusi Dmitry Muratov, ambaye pia ni mshindi wa tuzo la amani la Nobel, aliuza Tuzo lake la Amani la Nobel kwa kitita cha dola milioni 103.5 ili kuweza kusaidia watoto wakimbizi nchini Ukrain kutokana na uvamizi wa Urusi nchini humo.

Hiki ndicho kiasi kikubwa cha pesa ambacho medali ya Tuzo ya Nobel imewahi kupata katika mnada na ya juu zaidi ilikuwa dola milioni 4.76 mwaka 2014, wakati James Watson, mgunduzi mwenza wa muundo wa DNA, alipouza Tuzo yake ya Nobel ya 1962.

Utambulisho wa mnunuzi haukuthibitishwa na Heritage Auctions, lakini walidokeza kuwa mnunuzi huyo anatoka ng’ambo. Muratov amekuwa akikosoa sana utawala wa Urusi tangu mwanzo wa uvamizi huo, na tayari ametoa dola 500,000 kwa mashirika tofauti ya misaada.


Share this story

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Previous post FIFA : Unaweza kufungwa jela miaka 7 iwapo utapatikana ukifanya ngono nje ya ndoa wakati wa kombe la dunia, nchini Qatar
Next post Why KOT are crazy after Naomi Osaka launched a media company “Hana Kuma Media”