Viongozi wa Kilifi Watishia Kuharamisha Miraa Kufuatia Hatua Ya Serikali Kupiga Marufuku ‘Mnazi’

Share this story

Viongozi wa kaunti ya Kilifi wametishia kupiga marufuku Muguka, kufuatia marufuku ya hivi majuzi ya unywaji wa mvinyo unaojulikana kama ‘mnazi’ katika eneo hilo.

Wakizungumza katika eneo la Jaribuni katika Kaunti Ndogo ya Kauma mnamo Ijumaa, Machi 15, viongozi hao waliikashifu serikali kwa kukiita kinywaji hicho kuwa haramu katika msako wa hivi majuzi wa uvamizi wa pombe za kienyeji nchini.

Viongozi hao walibainisha zaidi kuwa Muguka, kichocheo kutoka eneo la Meru, kimeathiri vijana zaidi katika eneo hilo, kuliko pombe ya kienyeji ya tangu jadi.

Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Kaunti ya Kilifi Ibrahim Abdi Matumbo alieleza kuwa Mnazi ni kinywaji cha kijamii na kitamaduni, na kukipiga marufuku ni dharau kwa jamii ya Mijikenda.


Share this story

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Previous post US Lawmakers Block Funding for the Haiti Mission By Kenya
Next post Wagonjwa Wateseka Mombasa Huku Mgomo Wa Madaktari Ukiingia Siku Ya Pili