𝐓𝐚𝐬𝐧𝐢𝐚 𝐲𝐚 𝐟𝐢𝐥𝐚𝐦𝐮 𝐧𝐜𝐡𝐢𝐧𝐢 𝐓𝐚𝐧𝐳𝐚𝐧𝐢𝐚 𝐧𝐚 𝐰𝐚𝐟𝐮𝐚𝐬𝐢 𝐰𝐚 𝐁𝐨𝐧𝐠𝐨 𝐌𝐨𝐯𝐢𝐞 𝐡𝐚𝐩𝐨 𝐣𝐚𝐧𝐚 𝐰𝐚𝐥𝐢𝐚𝐝𝐡𝐢𝐦𝐢𝐬𝐡𝐚 𝐦𝐢𝐚𝐤𝐚 𝟏𝟎 𝐭𝐚𝐧𝐠𝐮 𝐤𝐢𝐟𝐨 𝐜𝐡𝐚 𝐒𝐭𝐞𝐩𝐡𝐞𝐧 𝐊𝐚𝐧𝐮𝐦𝐛𝐚.

Share this story

Hapo jana wafuasi wa bongo movie na mashabiki wa aliyekuwa movie star wa Filamu za kibongo marehemu Steven Kanumba, waliweza kuadhimisha mwongo mmoja tokea kufariki kwake

Steven Kanumba alizaliwa January 8, 1984, katika familia wa Wasukuma katika mkoa wa Shinyanga kaskazini mwa Tanzania. Alikuwa maarufu sana kwa kazi ya filamu na televisheni na kuitwa nyota maarudu zaid Tanzania (Steven Kanumba The Great)

Steven Kanumba Unfortunate Love Beat by Sina Tatizo Na Mtu on Amazon Music  - Amazon.com

Alifanya kazi nyingi ndani na nje ya nchi na amewahi fanya kazi na mwigizaji maarufu wa Nigeria Ramsey Nouah, filamu iliyotambulika kama ‘DEVILS KINGDOM’

Anatambulika kwa filamu nyingi za kiswahili kama Oprah, A Point of No Return, Lost Twins, Red Valentine, Love & Power, Neno La Mwisho, Big Daddy, Deception, The stolen will, Johari na zinginezo.

Alicheza filamu ya Love & Power na Ndoa Yangu mwaka wa 2012 kabla ya kifo chake

Kanumba ndiye mwigizaji wa kipekee nchini Tanzania aliyeshinda tuzo nyingi na taaluma yake ilichukua zaidi ya muongo mmoja. Baadi ya tuzo alizoshinda ni kama Muigizaji bora wa mwaka 2006, muigizaji bora Tanzania 2007, Tuzo ya msanii bora mwaka wa 2008

Elizabeth Michael Lulu sent to prison for the death of Steven Kanumba
Aliwahi kuwa mgeni maalum kwa shindani la Big Brother Africa 4 mwaka wa 2009 na pia kuteuliwa kuwa balozi wa OXFAM GROW nchini Tanzania mwaka wa 2011.
Kanumba alifariki tarehe 7 April, 2012 baada ya kusemakana alisukumwa na mpezi wake, Elizabeth Lulu, na kuanguka kufuatia ugomvi waliokuwa nao.

Share this story

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Previous post East African Community heads of state are in Nairobi, Kenya to witness the signing of the treaty of accession by the Democratic Republic of Congo to the EAC regional block.
Next post Chiloba Makes a U-Turn on Sim Card Registration, Says exercise not for all Kenyans