Raia wa Chad ambaye aliyemlaghai Seneta wa Tana River, Danson Mungatana, Shilingi Milioni 76 katika dili ghushi ya mafuta ameondolewa mashtaka.
Seneta wa Tana River Danson Mungatana apoteza ombi la kumtaka, Chadian Abdoulaye Tamba kufungwa jela kwa kumlaghai Ksh 76M.
Mahakama imemwachilia huru raia wa Chad aliyemlaghai Seneta wa Tana River Danson Mungatana shilingi milioni 76 katika kandarasi ghushi ya mafuta.
Abdoulaye Tamba, ambaye alishtakiwa mwaka 2018, alikutwa hana hatia kutokana na kukosekana kwa ushahidi na upande wa mashtaka kushindwa kuleta mashahidi wa kuthibitisha shtaka la kujipatia fedha kwa njia za uongo.
Hakimu wa mahakama hiyo Ben Mark Ekhubi hata hivyo alimpata na hatia ya kumiliki dola ghushi za Kimarekani na Euro. Mahakama ilisema mshtakiwa pia alipokea pesa kwa njia za uwongo kutoka kwa Makau Muteke. Upande wa mashtaka ulikuwa umeita mashahidi saba wakati wa kesi hiyo na Mungatana alikuwa shahidi wa kwanza wa upande wa mashtaka. Upande wa mashtaka uliomba kutayarisha ripoti ya awali ya hukumu na kesi hiyo kutajwa Novemba 9.