
Ofa Ya PSG Dhidi ya Yamal Yagonga Mwamba
Paris Saint-Germain (PSG) ilitoa ofa ya €250 milioni kwa ajili ya kutaka kumsajili Lamine Yamal kutoka FC Barcelona, lakini ofa hiyo imekataliwa.
Hata hivyo, nyota huyo raia wa Spain ameonyesha nia ya kuendelea kusalia katika klabu ya Barcelona.
Pia, wakala wake, Jorge Mendes, alithibitisha kuwa Yamal atabaki katika klabu ya Barcelona kwa miaka mingi ijayo.
#SRSportsUPDATES #LaLiga