Niffer amehamasisha Vurugu na kuharibu miundombinu- Polisi
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limethibitisha kumkamata na linamhoji Jenifer Bilikwiza Jovin almaarufu Niffer leo tarehe Oktoba 27, 2025 majira ya saa 9 mchana eneo la Sinza Kumekucha kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo kuhamasisha vurugu huku hatua zaidi za kisheria zikiendelea kuzingatiwa dhidi yake.
Taarifa ya leo Oktoba 27, 2025 iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Jumanne Muliro imebainisha kuwa Niffer 26, mkazi wa Masaki Peninsula Kinondoni amekamatwa kwa tuhuma za kuhamasisha vurugu na kuharibu miundombinu katika maeneo mbalimbali jijini humo hasa siku za kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025.
Haya yanajiri masaa kadhaa baada ya taarifa kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Mfanyabiashara huyo maarufu Nchini ametekwa na Watu wasiojulikana leo Oktoba 27, 2025 akiwa Dukani kwake maeneo ya Sinza Kumekucha Jijini Dar es salaam.
Kupitia Kitenge