Bunge lilipata hasara ya milioni 94 wakati wa maandamano
Spika wa Bunge la Kenya, Moses Wetang’ula amesema ghasia zilizoibuka kufuatia maandamano ya Gen Z ziliharibu vitu vyenye thamani ya karibu Shilingi milioni 94.
Watang’ula amewaambia wanahabari leo Julai 22, kuwa tathmini na uthamini huo ulifanywa na kampuni ya bima.
“Huo ndio uharibifu tulioupata. Kwa hivyo kampuni ya bima imeshughulikia suala hilo,” alisema.
Hata hivyo, walipa kodi hawataingia gharama yoyote kwani kampuni ya bima itachukua nafasi ya vitu vyote, ikiwa ni pamoja na kukarabati miundombinu iliyoharibika.
Wetang’ula amesema kuwa waandamanaji walivunja skrini za televisheni, vifaa na kuharibu majengo