Wakazi wa Mombasa waandamana kupinga Mswada wa Fedha 2024
Machafuko na mapigano yalitanda katika mitaa ya Mombasa siku ya Jumatano huku wakazi wakiandamana barabarani kupinga Mswada wa Fedha wa 2024.
Waandamanaji hao walikabiliana na maafisa wa polisi wa kupambana na ghasia ambao walikuwa wametumwa kudhibiti maandamano hayo.
Barabara na biashara zilisalia bila magari huku maduka yakiwa yamefungwa kwa sehemu bora ya Jumatano asubuhi.