MWANAMUZIKI “ZAHARA” ALIYEIMBA LOLIWE AFARIKI DUNIA
Muimbaji maarufu wa Afrika kusini Bulelwa Mkutukana maarufu kama Zahara amefariki Dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu maradhi ya Ini.
Zahara ambaye amezaliwa November 9 Mwaka 1987 amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya ini ambapo majuma mawili yaliyopita familia yake ilitoa taarifa kwa umma ya kuthibitisha hali ya binti yao na kwamba kwa Wakati huo alikuwa anaendelea na matibabu.
Wakati wa uhai wake Zahara amefanya kazi nyingi zilizotamba sana zikiwemo Loliwe, Destiny, Mgodi, Phendula, Ndiza na nyinginezo
R. I. P Zahara