Wasiwasi Wa Man City Kukosa Ligi Ya Mabingwa Msimu Ujao
Kocha wa Manchester City Pep Guardiola anasema klabu hiyo iko katika hatari ya kukosa nafasi ya kushiriki katika Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.
City kwa sasa wako katika msimu wao wa 14 mfululizo katika mashindano ya klabu bingwa barani Ulaya.
Ni Arsenal pekee kati ya 1998 na 2017, na Manchester United kati ya 1996 na 2014, ambazo ndizo zilizo na rekodi ndefu zaidi ya kufuzu kati ya vilabu vya Uingereza.
City wamo katika nafasi ya saba kwenye Ligi ya Premia baada ya mechi 17, pointi nne nyuma ya Nottingham Forest iliyo nafasi ya nne na pointi moja nyuma ya Bournemouth iliyo nafasi ya tano.
England kwa sasa wako kileleni mwa jedwali la Uefa la Uropa na wako katika nafasi nzuri ya kupata nafasi ya tano kwenye Ligi ya Mabingwa msimu ujao, ingawa City bado hawatafuzu kwenye msimamo wa sasa.
“Niliposema hapo awali, watu walicheka,” alisema Guardiola. “Walisema, ‘kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa sio mafanikio makubwa’.
“Lakini najua kwa sababu inatokea kwa vilabu katika nchi hii. Walitawala kwa miaka mingi na baada ya miaka mingi wakashindwa kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa.”