MZEE PEMBE AFARIKI DUNIA
Mchekeshaji mkongwe Tanzania Mzee Yusuph Kaimu maarufu kwa jina la “Mzee Pembe” amefariki dunia muda wa alasiri ya leo Oktoba 20, 2024.
Taarifa ya kifo chake imethibitishwa na baadhi ya wachekeshaji wenzie na wasanii wa filamu aliowahi kufanya nao kazi enzi za uhai wake na taratibu za mazishi zinafuata.