Mkongwe Wa Magari Suzuki Amefariki Dunia
Mfanyabiashara mkongwe wa Japan na Mwenyekiti wa zamani wa kampuni ya Magari ya Suzuki Motor Bw. Osamu Suzuki (94), amefariki dunia.
Suzuki aliyeiongoza Kampuni hiyo kwa zaidi ya miaka 40 alifariki Disemba 25, baada ya kuugua ugonjwa wa Saratani.
Atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa wa kuiongoza Kampuni hiyo kuingia India, na kuleta mapinduzi katika sekta ya Magari duniani