Lucia Witbooi Ateuliwa Kuwa Makamu wa Rais Katika Baraza la Mawaziri Nchini Namibia

Share this story

Rais mpya wa Namibia Netumbo Nandi-Ndaitwah amemteua Lucia Witbooi kuwa Makamu wa Rais katika Baraza la Mawaziri lililopunguzwa.

Nandi-Ndaitwah, ambaye aliapishwa Ijumaa baada ya chama chake, SWAPO kupata ushindi mwezi Novemba, pia alimtaja Natangwe Ihete kama Waziri wa Madini na Nishati na Selma Ashipala-Musavyi kama Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara.

Nandi-Ndaitwah, Rais wa kwanza Mwanamke wa Namibia, alipunguza Baraza lake la Mawaziri kutoka Mawaziri 21 na Manaibu 21 hadi Mawaziri 14 na Manaibu saba kwa kuunganisha baadhi ya ofisi na kuhamisha baadhi ya majukumu kwa Mawaziri.

Hatua hiyo inalenga kuondoa urudufishaji, kupunguza matumizi na kuhakikisha utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya Serikali kwa ufanisi na ukamilifu.


Share this story

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Previous post Harambee Stars lose 2-1 to Gabon in World Cup qualifier
Next post Pope Francis makes his first public appearance after spending several weeks in the hospital.