Kamanda mkuu wa Hezbollah auawa katika shambulizi la Israel huko Beirut

Share this story

BEIRUT: KUNDI la Hezbollah la Lebanon limethibitisha kuuawa kwa wanachama wake 16 wakiwemo kiongozi mwandamzi Ibrahim Aqil na kamanda mwingine Ahmed Wahbi katika shambulio la anga la jeshi la Israel mapema leo katika mji mkuu, Beirut.


Wizara ya Afya ya Lebanon imesema jumla ya watu 31 wameuawa wakiwemo watoto watatu na wanawake saba katika shambulio hilo baya zaidi katika mgogoro kati ya Hezbollah na Israel uliodumu kwa mwaka mmoja.


Shambulio hilo limezidisha mgogoro kati ya Israel na Hezbollah inayoungwa mkono na Iran na limeleta pigo kwa kundi hilo baada vifaa vya mawasiliano vya wanachama wake kulipuka wiki hii.
Idadi ya watu waliokufa kutokana na mashambulio ya vifaa hivyo vya mawasiliano imeongezeka na kufikia 39 na zaidi ya 3000 kujeruhiwa


Share this story

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Previous post David Beckham : Sababu Za Kumchagua Messi Badaya Ya Cristiano
Next post Academy of Achievement Awards Faith Kipyegon and Beatrice Chebet in New York