Ajali Mbaya Eneo La Maungu Baadhi Ya Wanafunzi Wapoteza Maisha
Wanafunzi kadha wa Kenyatta wahofiwa kupoteza maisha baada ya ajali ya barabara eneo la Maungu Kaunti ya Taita Taveta.
Ajali hiyo ilitokea wakati basi lililokuwa limebeba wanafunzi wa Afya ya Umma lililokuwa likitoka Mombasa Safari kuelekea Nairobi kugongana na trela.
Juhudi za kuwanusuru waliopata ajali zinaendelea majeruhi wakikimbizwa Hospitali ya rufaa ya Moi mjini Voi.