๐Œ๐œ๐ก๐ž๐ณ๐š๐ฃ๐ข ๐ฐ๐š ๐๐ซ๐š๐ณ๐ข๐ฅ, ๐‘๐จ๐ง๐š๐ฅ๐๐จ ๐‹๐ฎรญ๐ฌ ๐๐š๐ณรก๐ซ๐ข๐จ ๐๐ž ๐‹๐ข๐ฆ๐š .

Share this story

Ni mwanasoka wa kulipwa aliyestaafu ambaye alicheza kama mshambuliaji akijulikana sana katika mpira wa kombe la dunia
Anachukuliwa kuwa mmoja wa wachezaji bora wa wakati wote. Akiwa mshambuliaji mahiri aliyeleta sura mpya kwenye nafasi hiyo, Ronaldo amekuwa na ushawishi kwa kizazi cha washambuliaji waliofuata. Sifa zake binafsi ni pamoja na kuchaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Dunia wa FIFA mara tatu na kushinda tuzo mbili za Ballon d’Or.

Ronaldo aliichezea Brazil katika mechi 98, akifunga mabao 62 na ndiye mfungaji wa tatu kwa timu ya taifa ya Brazil. Akiwa na umri wa miaka 17, alikuwa mchezaji mdogo zaidi wa kikosi cha Brazil kilichoshinda Kombe la Dunia la FIFA la 1994. Katika Kombe la Dunia la FIFA la 1998, Ronaldo alipokea Mpira wa Dhahabu kama mchezaji bora wa michuano hiyo baada ya kuisaidia Brazil kufika fainali, ambapo alipatwa na mshtuko wa moyo saa chache kabla ya mchuano kuanza. Alishinda Kombe la Dunia la FIFA la 2002,.
Alikuwa mshambuliaji hatari akishirikiana na Ronaldinho na Rivaldo.

Februari 2011, baada ya klabu ya Corinthians kuondolewa kwenye Copa Libertadores 2011 na timu ya Deportes Tolima ya Colombia, Ronaldo alitangaza kustaafu soka, akihitimisha miaka 18 ya maisha yake kwa mpira wa soka.

Kwa sasa Ronaldo ni mfanyabiashara , rais wa klabu ya La Liga Real Valladolid na mmiliki wa klabu ya Brasileiro Sรฉrie B Cruzeiro
Mnamo Septemba 2018, Ronaldo alikua mmiliki mkubwa wa kilabu cha La Liga, Real Valladolid baada ya kununua 51% ya hisa za kilabu kwa Euro milioni 30.

Ili kupata habari zaidi za Spoti tembelea channel yetu ya instagram yetu https://t.me/ngasumedia


Share this story

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Previous post Tazama kilichomtokea huyu bondia wa Tanzania mwenye ngumi ya ndoige
Next post Governor Mwadime Holds Meeting With Nacada Board Led By Chair Prof Mabel Imbuga & CEO Victor Okioma At Mombasa