Mwana FA na AY washinda rufaa fidia dhidi ya Tigo
Mahakama ya Rufaa Tanzania imewapa ushindi wasanii wa muziki wa kizazi kipya, Hamis Mwinjuma (Mwana FA) na Ambwene Yesaya (AY), katika rufaa ya muda mrefu dhidi ya kampuni ya mawasiliano ya Tigo (sasa ikifahamika kama Honora), kuhusu matumizi yasiyoidhinishwa ya kazi zao za muziki.
Mahakama ya Rufaa imebatilisha uamuzi huo uliokuwa umefuta fidia ya zaidi ya TZS bilioni 2.1 iliyokuwa imeamriwa na Mahakama ya Wilaya ya Ilala mwaka 2016, ikisema kuwa Mahakama ya Wilaya ilikuwa na mamlaka halali kusikiliza na kutoa uamuzi kuhusu shauri hilo.
Wasanii hao walifungua kesi hiyo wakidai kuwa nyimbo zao zilitumika na kampuni hiyo bila ridhaa yao. Mahakama ya Ilala ilikubaliana na hoja zao na kuamuru walipwe fidia ya TZS bilioni 2.16 kama hasara maalum pamoja na TZS milioni 25 kama fidia ya jumla.