
Africa Mashariki Imezindua Mfumo Wa Dhamana wa EACBond
Jumuiya ya Afrika Mashariki, EAC leo imezindua 𝑬𝑨𝑪𝑩𝒐𝒏𝒅, dhamana ya kikanda ya udhamini wa biashara.
Hatua hiyo, inachukua nafasi ya hitaji la dhamana nyingi za kitaifa wakati wa kusafirisha bidhaa katika nchi wanachama.
Jumuiya hiyo inasema kuwa EACBond itapunguza kwa kiasi kikubwa gharama za biashara, kupunguza ucheleweshaji mipakani na kukomboa mtaji wa biashara.