Pep Guardiola ameachana rasmi na mke wake Cristina Serra
Kocha mkuu wa Manchester City ya Uingereza Pep Guardiola ameachana rasmi na mke wake Cristina Serra baada ya kudumu kwenye ndoa miaka 30. Katika talaka waliyopeana mahakamani mke huyo wa Guardiola atatwaa nusu ya utajiri wa Guardiola na jumba lake kubwa la kifahari lililopo jijini Manchester nchini Uingereza.
Sababu kuu ya mke huyo kuomba talaka ni Guardiola kuwa bize mno na masuala ya mpira na kukosa muda na familia. Guardiola na mke wake huyo katika miaka 30 ya ndoa wamefanikiwa kupata watoto watatu Marius, Maria na Valentina
Inasemekana kwa takribani miaka mitano sasa walikua hawaishi pamoja, mke alikuwa anasimamia biashara zake za mitindo (fashion) huku mumewe akiwa bize na soka