Yanga Yapokea Kichapo Dhidi Ya MC Alger
Yanga inapoteza mechi ya pili mfululizo ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kupokea kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya MC Alger.
FT : MC Alger 2-0 Yanga SC
Ayoub Abdellaoui
Sofiane Bayazid
Yanga SC ilicheza ugenini nchini Algeria na MC Alger katika Uwanja wa 5 July 1962 kusaka alama tatu muhimu ikiwa ni mchezo wa pili wa hatua ya Makundi ya Klabu Bingwa Afrika.
Yanga ilikuwa imepoteza kwa 2-0 katika mchezo wa awali nyumbani dhidi Al Hilal ya Sudan.