Urusi : Rais Wa Urusi, Vladimir Putin Amuunga Mkono Kamala Harris’
Urusi inamuunga mkono Kamala Harris’: Historia ya Putin ya ‘maidhinisho ya uchaguzi wa Marekani
Rais wa Urusi, Vladimir Putin amesema baada ya Rais wa sasa wa Marekani, Joe Biden kujiondoa katika kinyang’anyiro cha Urais, Taifa la Urusi linamuunga mkono Makamu wa Rais Kamala Harris ambaye amemrithi Biden katika tiketi ya Urais kupitia Chama cha Democratic.
Akizungumza katika kongamano la kiuchumi katika Mji wa Vladivostok, Putin amesema “tuliyempenda zaidi nikisema hivyo alikuwa Rais wa sasa Biden aliyeondolewa kwenye kinyang’anyiro lakini alipendekeza Wafuasi wake wote wamuunge mkono Harris, hilo ndilo tutafanya pia.” amesema.
Hata hivyo ameongeza kuwa “muhimu zaidi ni chaguo la Watu wa Amerika na sio kile ambacho Urusi inafikiria au kuunga mkono,” kauli hiyo imepokelewa vibaya na John Kirby, Msemaji wa Baraza la Usalama la Marekani ambaye amemtaka Kiongozi huyo kuacha kuingilia uchaguzi wa Nchi hiyo.
Hii sio mara ya kwanza kwa Putin kumuunga mkono Mgombea wa Urais wa Marekani, mwaka 2004 Rais huyo alitangaza kumuunga mkono Rais aliyemaliza muda wake kupitia Chama cha Republican George W Bush ambaye alishinda katika uchaguzi huo kwa tofauti ndogo ya kura 35 dhidi ya John Kerry wa Democratic.