UGOMVI WA MESSI, NEYMAR NA MBAPPE ULIKUWA WIVU TU

Share this story

MSHAMBULIAJI wa timu ya taifa ya Brazil Neymar ameweka wazi kwa nini ushirikiano wa nyota watatu – yeye, Kylian Mbappe, na Lionel Messi haukufaulu kama ilivyotarajiwa katika klabu ya Paris Saint-Germain (PSG). Akizungumza na Romário, Neymar alisema kwamba ujio wa Messi ulisababisha ‘wivu’ na ‘mabadiliko ya tabia’ kutoka kwa Mbappe, huku akieleza kuwa ‘ego’ (kujiona/kujiskia) zilizuia timu kufikia mafanikio.

Alipoulizwa na Romario kama Mbappe ni mtu ‘anayekera,’ Neymar alisema:

“Hapana, si mtu wa kukera.Tuliwahi kugombana kidogo, lakini alikuwa muhimu sana kwetu alipowasili. Nilikuwa nikimuita ‘Golden Boy.’ Nilikuwa nikicheza naye, nikimwambia atakuwa mmoja wa wachezaji bora. Nilimsaidia kila mara, nilizungumza naye, alikuja nyumbani kwangu na kula chakula cha jioni pamoja”.

“Tulikuwa na miaka mizuri ya ushirikiano, lakini baada ya Messi kuja, alikuwa na wivu kidogo. Hakutaka kunishirikisha na mtu yeyote. Ndipo ugomvi ulipoanza na tabia zikaanza kubadilika,” alisema Neymar.

Ujio wa Messi mwaka 2021 ulionekana kukamilisha safu ya mashambulizi yenye vipaji vya hali ya juu, lakini PSG haikuweza kufanikisha lengo lake la kushinda taji la kwanza la Ligi ya Mabingwa.

Messi alijiunga na Inter Miami kunako MLS baada ya mkumalizika kwa mashindano ya Kombe la Dunia huku Mbappe akiondoka PSG kiangazi kilichopita na kujiunga na Real Madrid. Neymar, ambaye alihamia Al Hilal mwaka 2023, alikumbwa na majeraha ya muda mrefu ambayo yamechelewesha kurejea kwake uwanjani na sasa kuna tetesi kwamba ataondoka klabuni hapo na kwenda kucheza nchini kwake Brazil au MLS.


Share this story

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Previous post  UDA Party Formally Merges With Mudavadi’s ANC