Pigo kwa Man City : Rodri atakuwa nje kwa muda mrefu kutokana na jeraha baya la goti
Manchester City imepata pigo kubwa baada ya ripoti kuibuka kuhusu jeraha alilopata Rodri kwenye sare na Arsenal.
Habari mbaya mno kwa bingwa mtetezi wa Premier League Manchester City baada ya ripoti kudai kwamba kiungo wa Uhispania Rodri atakosa salio la msimu kufuatia jeraha alilopata dhidi ya Arsenal kwenye sare ya 2-2 ugani Etihad.
Rodri amefanyiwa vipimo na kuonyesha kwamba hataweza kuendelea kuwatumikia vijana hao wa kocha Pep Guardiolla. Rodri anatarajiwa kurudi uwanjani msimu wa 2025/2026.
The Gunners walilazimishwa suluhu ya pointi moja katika sare ya 2-2 na City Jumapili alasiri katika Ligi ya Premia. Riccardo Calafiori na Gabriel Magalhaes walifunga mabao ya Arsenal ambayo yalitosha kuona timu ya Mikel Arteta ikipata pointi zote tatu baada ya Erling Haaland kufunga bao la kwanza.