Gachagua avunja ukimya kuhusu madai ya Malala kuasi DCP
Aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua amezungumzia tetesi zinazoongezeka kuhusu aliko Cleophas Malala, naibu kiongozi wa Chama cha Demokrasia kwa Wananchi (DCP) na mmoja wa washirika wake wa karibu wa kisiasa. Katika mahojiano na kituo kimoja cha redio Jumapili, Januari 18, 2026, Gachagua alipuuzilia mbali ripoti zinazodai kuwa Malalah aliachana na kambi yake ya kisiasa baada ya kukosa kuhudhuria mafungo ya chama huko Mombasa, akielezea madai hayo kama propaganda za kupotosha.
Gachagua alisema naibu wake aliugua homa hiyo akiwa Kakamega na kuchukua likizo ya ugonjwa, akipuuzilia mbali madai ya kuasi chama.