Paul Biya ashinda urais Tena akiwa na umri wa miaka 92

Share this story

Rais wa Cameroon mwenye umri wa miaka 92 ameshinda kura ya uraisi kwa muhula wa nane uliokumbwa na utata.i.

Paul Biya, ambaye ni mkuu wa nchi mwenye umri mkubwa zaidi duniani, alipata 53.7% ya kura, ikilinganishwa na 35.2% ya kiongozi wa upinzani Issa Tchiroma Bakary, Baraza la Katiba lilitangaza.

Kabla ya tangazo hilo, Tchiroma Bakary – mshirika wa zamani wa Biya – alisisitiza kuwa ameshinda uchaguzi huo, lakini chama tawala cha Cameroon People’s Democratic Movement (CPDM) kilitupilia mbali madai yake.

Uchaguzi huo, uliofanyika tarehe 12 Oktoba, umekumbwa na ghasia mbaya, na katika siku za hivi karibuni, mamia ya wafuasi wa Tchiroma Bakary wamekaidi marufuku ya maandamano katika miji kadhaa, na kukabiliana na vikosi vya usalama.


Share this story

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Previous post Hali Ya Ati Ati Yashuhudiwa Mpaka wa Njukini na Elerai
Next post 12 feared Dead after a Plain crashed shortly after takeoff from Diani, Kwale