Mwanasoka nguli wa Man Utd na Scotland Dennis Law afariki akiwa na umri wa miaka 84
Mshambuliaji Nguli wa zamani wa zamani wa Manchester United timu ya Taifa ya Scotland, Dennis Law amefariki Dunia leo Januari 17, 2025 akiwa na umri wa miaka 84.
Law ambaye ni mchezaji wa kwanza wa Manchester United kushinda tuzo ya Ballon d’Or mnamo mwaka 1964 aliifungia klabu hiyo jumla ya magoli 237 kwenye mechi 404 akihudumu klabuni hapo kwa kipindi cha miaka 11.
Manchester United ina huzuni kubwa kushiriki taarifa ifuatayo kwa niaba ya familia ya Sheria:
“Ni kwa moyo mzito tunakuambia baba yetu Denis Law amefariki dunia kwa huzuni. Alipigana vita vikali lakini hatimaye sasa ana amani.
“Tunapenda kumshukuru kila mtu ambaye alichangia ustawi na utunzaji wake, zamani na hivi karibuni zaidi.
“Tunajua jinsi watu walivyomuunga mkono na kumpenda na kwamba upendo ulithaminiwa kila wakati na kuleta mabadiliko. Asante.”
Nyota huyo ambaye amewahi kuchezea Huddersfield, Manchester City na Torino ni mchezaji wa tatu mwenye magoli mengi zaidi kihistoria ndani ya klabu ya Manchester United nyuma ya Wayne Rooney na Sir Bobby Charlton.
Law almaarufu ‘The King’ au ‘Lawman’ alikuwa Nguli pekee aliyesalia kwenye utatu maarufu wa Manchester United wa George Best, Dennis Law na Bobby Charlton wanaoonekana kwenye sanamu la watu watatu pichani.