Naibu Rais, Rigathi Gachagua amekana madai ya kumtaka Rais William Ruto kumpa Ksh. Bilioni 8
Naibu Rais, Rigathi Gachagua amekana madai ya kumtaka Rais William Ruto kumpa Ksh. Bilioni 8 (takriban Tsh. Bilioni 168) ili akubali kuachia nafasi hiyo kutokana na Wawili hao kutokuwa na uhusiano mzuri
Akihojiwa na kituo cha Redio, amesema “Sina tamaa ya fedha, ningekuwa nazitaka ningenunuliwa na Wapinzani ili nitengane na Rais Ruto, sina tamaa, Watoto wangu ni wakubwa, Mke wangu ni Mchungaji, fedha sio chaguo langu la Kwanza, Wakenya ndio kipaumbele changu.”
Ikumbukwe, Muswada wa kumng’oa Gachagua kwenye nafasi ya Naibu Rais unatarajiwa kuwasilishwa Bungeni kesho Oktoba Mosi, 2024 kutokana na shutuma kadhaa ikiwemo kuchochea chuki kwa Wananchi, kueneza Ukabila na Ufisadi