Watu Watatu Waelekea Mahakamani Kupinga Azma Ya Ruto Kuwa Rais
Watu watatu wamepeleka ombi mahakamani kuzuia naibu rais kugombania kiti cha uraisi mwaka mwezi wa Agosti.
Wanaharakati hao wanataka mahakama imzue naibu raisi kugombania kiti kwa madai ya kuwa kiti cha naibu wa raisi na kile cha uraisi kinachaguliwa wakati mmoja na inawalazimu kumaliza muhula waliotengewa na katiba.
Watatu hao walisema kuwa mahakama inapaswa kuiona kuwa ni lazima kwamba viongozi wawili wa kisiasa wanapaswa kustaafu baada ya muhula wao kuisha.
Tume ya Uhuru na Mipango ya Uchaguzi (IEBC), pia ilikuwa imejumuishwa kwa kesi kama mhojiwa. Onyango na waombaji wengine wawili wanataka tume inayoongozwa na mwenyekiti wake Wafula Chebukati kusimamishwa kuandikisha maafisa wa serikali kwa mchakato wa uchaguzi.