Kalonzo : Hatutatia saini ripoti hadi mahitaji ya watu yatimizwe
Kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka amesema upande wa Azimio-One Kenya Alliance haitatia saini ripoti yoyote hadi pale mahitaji ya watu yatatimizwa.
Akizungumza Jumapili huko Vihiga, alisema iwapo matarajio ya Wakenya hayatatimizwa, upande unaongoza mazungumzo wa Azimio hautaruhusu ripoti hiyo kutumwa kwa Bunge la Kitaifa.
“Kwa sababu bila sisi kutia saini, haitafika Bungeni. Ni wazi tusipotia saini, haiwezi kutumwa kwa bunge. (Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna),” alisema.
Kalonzo, ambaye ni mwenyekiti wa timu ya mazungumzo ya Azimio, alisema watawapa Wakenya vipaumbele katika mchakato wa kuandika ripoti hiyo.
“Kwa hivo mambo haya mazungumzo pasipo cost of living-gharama ya maisha kuja chini, there is no dealĀ (So in these things, these talks, without the lowering of the cost of living there is no deal),” he said.