𝐖𝐀𝐊𝐔𝐉𝐀𝐀 𝐀𝐎𝐍𝐆𝐎𝐙𝐀 𝐕𝐈𝐎𝐍𝐆𝐎𝐙𝐈 𝐊𝐖𝐀 𝐊𝐈𝐊𝐀𝐎 𝐍𝐀 𝐍𝐀𝐈𝐁𝐔 𝐑𝐀𝐈𝐒.
Viongozi wa kaunti ya Taita Taveta leo wamekutana na Naibu Rais jijini Nairobi kwa kikao maalum cha kujadili uboreshaji ushirikiano kati ya serikali kuu na serikali ya ugatuzi ili kufanikisha maendeleo ya kaunti hii.
Masuala yaliyopewa kipaumbele ni pamoja na sekta ya afya, maji, madini, miundombinu, na elimu. Uongozi wa Taita Taveta, chini ya H.E Dr. Andrew Mwadime – Wakujaa, EGH, Governor Taita Taveta County, umeweka wazi umuhimu wa kuimarisha utoaji huduma na maendeleo katika maeneo haya. Aidha, wito umetolewa kwa serikali ya Kenya Kwanza kutimiza ahadi za maendeleo zilizotolewa kwa kaunti hiyo.