Nitarejea kwenye uinjilisti nikistaafu – Raisi Ruto
Rais wa Kenya, William Ruto amesema atarejea kwenye kazi yake ya kumtumikia mungu kama mwinjilisti baada ya kumaliza muhula wake wa kuongoza Kenya kama Rais.
“Nitarejea kwenye uinjilisti nitakapomaliza wajibu wangu kama Rais,” Ruto amesema wakati wa ibada katika Kaunti ya Bungoma siku ya Jumapili akidokeza mpango wake baada ya kustaafu.
Rais Ruto alidai kwamba malezi yake yalijikita katika kujifunza na kufundisha neno la Mungu na atalirudia baada ya kuacha urais.