Imam Khamenei alimtunuku “Nishani ya Fath” Brigedia Jenerali Amir Ali Hajizadeh, kamanda wa Kikosi cha Wanaanga wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Leo kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khemenei amemvisha nishani ya heshima kamanda mkuu wa jeshi la anga la nchi hiyo Brigedia Jenerali Amir Ali Hajizadeh ambaye ndiye aliyeratibu mashambulizi dhidi ya Israel tarehe 1 mwezi huu yaliyopewa jina “Operesheni Ahadi ya Kweli 2″(Operation True Promise 2)
Amir anatajwa kwamba ndiye aliyeratibu pia mashambulizi dhidi ya Israel mwezi Aprili mwaka huu yaliyopewa jina “Operesheni Ahadi ya Kweli”
Baada ya kuuawa kamanda mkuu wa vikosi vya mapinduzi ya Iran “IRGC” Jenerali Qasim Soleiman na vikosi vya Marekani mwaka 2020, Amir anatajwa kuwa ndiye aliyeratibu pia mashambulizi ya kulipa kisasi dhidi ya kambi za Marekani nchini Iraq, operesheni aliyoipa jina “Shujaa Soleiman”(Matyr Soleiman). Jenerali huyu ni moja ya makamanda waliowekewa vikwazo na Marekani.
Wiki hii Iran imeendelea na shamra shamra za kujivunia mashambulizi makubwa zaidi dhidi ya Israel mapema mwezi huu ambayo kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khemenei ameyaita mashambulizi halali yaliyofanikiwa dhidi ya adui
Hayo yanaendelea wakati Israel ikiwa imeapa italipa kisasi cha aina yake ndani ya muda wowote.
Duru mbalimbali zinaeleza huenda shamra shamra hizo zikakumbwa na kadhia muda wowote kutokana na historia ya Israel dhidi ya wote wanaoshiriki katika mipango ya kuishambulia, hivyo ni vyema dua nyingi zikaelekezwa kwake.
Iran yenyewe imesema ipo imara kukabili kitisho chochote kutoka Israel na imeapa kutoa majibu makali zaidi
Picha kwa hisani ya Telegraph
Amir ni moja kati ya makamanda wakubwa wanaoheshimika mno nchini Iran baada ya marehemu Qasim Soleiman aliyeuawa na vikosi vya Marekani mwaka 2020 nchini Syria