Hatuna ugomvi ni ushindani wa kazi – Ali Kiba
MSANII wa Bongo fleva Ali Kiba amesema kuwa hakuna ugomvi baina yake na msanii mwenzake Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ bali ni ushindani wa kazi zao ndio maana wanaona kama kuna chuki baina yao.
King Kiba Amezungumza hayo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Crown Tv.
“Sijawai kusema wala kumwambia mtu kuwa nina ugomvi na msanii mwenzangu yeyote labda ushindani wetu wa biashara ndio sababu watu wanasema maneno yao wenyewe.
Pia ameongeza kuwa Msanii wa lebo ya Wasafi Mbosso Khan na Abdul Kiba ni marafiki kabla hata Mbosso kuwa kwenye lebo hiyo, hivyo wao kufanya kazi amebariki.
“Sitamzuia msanii wa Kings Music kufanya kazi na msanii yeyote, kinachotakiwa ni kazi nzuri ambayo inaingiza pesa kwenye lebo na kuwapa mashabiki muziki mzuri.”amesema Alikiba.